Afrique
Sous catégorie
Mizinga ikipigwa katika mazishi ya Edward Lowassa
Mwili wa Hayati Lowassa ukishushwa kaburini na wanajeshi wa JWTZ
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Kiongozi wa Chama ACT Wazalendo Zitto Kabwe wakiungana na wanafamilia kutoa heshima za mwisho. #EdwardLowassa #Lowassa
Familoa ya marehemu Edward Lowassa ikitoa heshima za mwoisho #Lowassa #EdwardLowassa
ABC & STALLION ZAUNGANA KUTAFUTA SULUHU NA HAKI ZA KISHERIA! | FURSA KWA WAWEKEZAJI!
Fredrick Lowassa ambaye ni mtoto wa kwanza wa marehemu Edward Lowassa akizungumza mengi yanayomhusu baba yake wakati wa uhai wake #Lowassa #EdwardLowassa
“Ukimzungumzia Lowassa Hayati wetu mpendwa, huwezi kutofautisha kumzungumzia katika muktadha wa kiutendaji wa serikali lakini pia mwanasiasa mahiri, sisi wanasiasa tunalo la kujifunza. Moja, katika utumishi wa umma na hasa ukizungumzia muktadha wa kisiasa, ni muhimu sana kuelewa kwamba unapokuwa mwanasiasa, utakabiliana na changomoto nyingi jambo muhimu ni lazima uwe ngozi ngumu, Mzee Lowassa ni kielelezo sahihi cha wanadamu hapa duniani wenye ngozi ngumu.” - William Mganga Ngeleja, aliyekuwa Mbunge wa Sengerema akimzungumzia Hayati Edward Lowassa.
Team ya Clouds 360 imehudhuria shughuli ya kuagwa kwa Hayati Edward Lowassa na Kuzungumza na Baadhi ya Viongozi wa Serikali waliopata fursa ya kuelezea walivyomfahamu Hayati.
“Ndg. Edward Lowassa, kwa maisha yake amekuwa akifanya kazi za kisiasa hakuna wakati aliojiriwa njee ya siasa isipokuwa, alipokuwa mwanajeshi wa jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania ambapo napo palikuwa ni chuo cha siasa, baada ya kutoka huko amefanya kazi katika jumuiya ya vijana wa Chama cha Mapinduzi, na amehudumu huko kwa mda mrefu zaidi lakini alipoingia katika siasa za ushindani alienda kuchaguliwa kuwa mbunge wa Monduli na akawa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, wakati wa awamu ya pili chini ya Waziri Mkuu, Malecela. Wakati anafanya kazi pale mimi nilikuwa mkuu wa mkoa wa Pwani, tuliwahi kusafiri nae kwa Helicopter mkoa mzima wa Pwani , tukitazama hali ya chakula, namfahamu namna hiyo alikuwa mtu wa kujituma kwa mambo aliyokabidhiwa kufanya.” - Stephen Wasira, Mwanasiasa Mkongwe akimzungumzia namna anavyomjua Hayati Edward Lowassa.
Kurejea kwa Hayati Edward Lowassa ndani ya Chama Cha Mapinduzi kulipokelewa kwa mshtuko na wengi, @kijahyunus amemuuliza Mzee Hamis Mgeja mmoja ya watu wa karibu wa Lowassa ambaye pia alihamia nae CHADEMA ni kitu gani kilisababisha arejee #LeigwananiEdo
Historia ya Edward Lowassa, Waziri Mkuu maarufu zaidi Tanzania na aliehudumu kipindi kifupi zaidi kama inavyosimuliwa na Caloriny Francis ikiwa imeandikwa na Ignas #EdwardLowassa #Lowassa
Aliewahi kuwa Naibu Waziri wa Elimu wakati Lowassa akiwa Waziri Mkuu Mwantum Mahiza akizungumzia utendaji wa marehemu enzi za uongozi wake kama Waziri Mkuu #EdwardLowassa #Lowassa
Balozi Adadi Mohamed Rajab akimzungumzia marehemu Edward Lowassa alivyokuwa mchapakazi wakati akiwa Waziri wa Maji #EdwardLowassa #Lowassa