Beatrice Chebet aweka historia jijini Paris
0
0
10/08/24
Ikiwa imesalia siku moja kabla ya makala ya 33 ya michezo ya olimpiki kukamilika jijini Paris ufaransa, Kenya imefanikiwa kunyakua medali saba, nne za shaba, fedha moja na mbili za dhahabu. Aliyenyakua nishani hizo za dhahabu ni Beatrice Chebet ambaye jana usiku aliandikisha historia ya kuwa mwanariadha wa kwanza wa kike nchini kushinda mbio za mita elfu kumi katika michezo ya olimpiki.
Montre plus
0 commentaires
sort Trier par