Suivant

Chama cha KUPPET, kimesema kitapambana na tume ya kuajiri walimu TSC kortini

29/08/24
K24 TV
Dans Afrique / Kenya

Chama cha walimu wa shule za upili, KUPPET, kimesema kitapambana na tume ya kuajiri walimu TSC kortini endapo tume haitatia saini mkataba wa kurejea kazini. Walimu hao wameishtumu TSC kwa kutumia mabavu kupitia mahakama huku wakisema mgomo wa walimu bado utaendelea, pia wamezidi kulalamika kuwa ingawa serikali imewasilisha shilingi bilioni 13.5 kwa utekelezwaji wa mkataba wa mwaka 2021 hadi mwaka wa 2025, bado kuna masuala katika mkataba huo ambayo hayajatekelezwa. wakati huo huo muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini (COTU) umeinyooshea tsc kidole cha lawama kuhusu mgomo huo. COTU inashauri TSC iwe na maafikiano na walimu.

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par


Suivant