Suivant

Chama cha Wiper chakanusha madai kuwa kina mazungumzo na Rais Ruto

24/07/24
K24 TV
Dans Afrique / Kenya

Chama cha Wiper kimekanusha madai kuwa kina mazungumzo na rais William Ruto katika kuunda serikali pana yenye kujumuisha wengi kwa ajili ya manufaa ya taifa na kushikilia kuwa azimio haitajiunga na serikali ya rais. Kwa upande wake ODM, imedai kuwa mwanachama yeyote wa ODM atakayetaka kujiunga na baraza la mawaziri la rais Ruto atakuwa anafanya hivyo bila baraka za chama. ODM kupitia taarifa ya katibu mkuu wa chama hicho, Edwin Sifuna amesema chama hakina mipango yoyote ya kisiasa na utawala wa sasa.

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par


Suivant