Suivant

FIRST YEAR 2024 WAFANYA ZIARA YA IJUE DAR TOUR

12/11/24
CLOUDSMEDIA
Dans Afrique / Tanzanie

Wanafunzi takribani wapya wa mwaka wa kwanza kwa vyuo vyote vilivyopo jijini Dar es salaam hususani wale wanafunzi wageni watokao nje ya Dar es Salaam, wamepata fursa ya kutembezwa maeneo mbalimbali kwa lengo la kulifahamu vizuri jiji. Wanafunzi hao wametembelea maeneo kama uwanja wa Benjamin Mkapa, daraja la Nyerere (Kigamboni), kituo kipya cha treni ya umeme (SGR), Posta mpya na ya zamani, Ikulu, daraja la Tanzanite pamoja na Coco beach. Ziara hiyo imeratibiwa na kanisa la Dar es Salaam Pentecostal Church (DPC), ikipewa jina la IJUE DAR katika mpango wake wa kuwakaribisha, kuwapokea, kuwaonesha na kuwafundisha vijana juu ya mambo mazuri yaliyopo Dar es Salaam na kutumia fursa hiyo kuwakanya kujiepusha na mambo mabaya yaliyo kinyume na maadili. Katika ziara hiyo kanisa la Dar es Salaam Pentecostal Church @dpc_tz imewakutanisha wanafunzi toka madhehebu na dini tofauti.

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par


Suivant