FULL INTERVIEW: TEAM LISSU NA TEAM MBOWE KUMEWAKA | HATUJAROGWA CHADEMA
"Utakumbuka Makamu Mwenyekiti (Tundu Lissu) akieleza kwamba kuna fedha nyingi. Alisema tu nyingi, hakutaja figure. Nafikiri ni mtu anayeelewa implications, ukitaja figure maana yake unaweza kutuambia mpaka muamala ilikuwa Saa ngapi, lini. Ukitoka kwenye akaunti ipi na kwenda kwenye akaunti gani? Na Mimi nime- demand kwa katibu Mkuu wa Chama kwamba Lyenda aitwe akadhibitishe. Lumola Stive– Kutoka team Mbowe akitoa tuhuma kwa mmoja wa timu Lissu, Gerva Lyenda alisema kuwa kuna Tshs zaidi ya Mil. 300 zinazodaiwa ni rushwa wakiwatuhumu timu ya Mbowe kuhusika na fedha hizo. #PBCloudsFM #GenCForLife Kwa kinachoendelea CHADEMA kwenye mvutano mkali wa Team Lissu na Mbowe, @masoudkipanya ameuliza vipi CHADEMA wamerogwa? Hapa kwenye #PBCloudsFM tupo na timu mbili; Gerva Lyenda – Kutoka Team Lissu (alikuwa Mtia nia ya Uenyekiti CHADEMA Kanda ya Pwani) na Lumola Stive– Kutoka team Mbowe (alikuwa Mgombea jimbo la Bukeni) Wamethibitisha kwamba wako salama, na hawajarogwa! Wewe unaonaje? Wako salama⁉️ #PBCloudsFM #GenCForLife