Suivant

Gavana wa Mombasa amhimiza Rais Ruto atekeleze ahadi yake

29/07/24
K24 TV
Dans Afrique / Kenya

Viongozi wa chama cha ODM wanazidi kushinikiza kuwa familia za waliopoteza maisha yao na majeruhi wakati wa maandamano ya Gen Z walipwe fidia na zaidi kutengwe siku ya kitaifa ya maombolezi. Gavana wa Mombasa abdulswamad Shariff Nassir amemtaka rais William Ruto ahakikishe haki inapatikana na kusiwe na ahadi hewa. Nassir vilevile ametaka matakwa yote ya chama cha ODM yatimizwe ikiwemo kuwaachilia mara moja wote waliokamatwa na kesi kuondolewa kwa ambao tayari wamefunguliwa mashtaka.

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par


Suivant