Kinara wa ODM Raila Odinga awakemea viongozi wa Kenya Kwanza
0
0
04/03/24
Kinara wa ODM Raila Odinga amewakemea viongozi wa Kenya Kwanza kwa kile ametaja kama unafiki baada ya kupitisha sheria ya fedha ya mwaka wa 2023 iliyoongeza ushuru na kuchangia katika kupanda kwa gharama ya maisha. Odinga anasema kuwa alisutwa kutokana na pingamizi yake ya sheria hiyo na kuonya wabunge wake dhidi ya kuunga mkono na anashangazwa na mabadaliko ya maono ya wabunge wa Kenya Kwanza huku akishikilia kuwa lazima washirikishwe katika kuidhinisha makamishna wapya wa IEBC. Mpasuko ndani ya Azimio umedhihirika wazi hii leo baada ya viongozi wa ODM kuukaripia upande wa Kalonzo Musyoka kwa juhudi za kutaka kumrithi Odinga kabla ya kuondoka kwake
Montre plus
0 commentaires
sort Trier par