Suivant

LIVE: Israel Mwenda Arejee Kambini Singida BS | Hili Game Ya CloudsFm

03/09/24
CLOUDSMEDIA
Dans Afrique / Tanzanie

Uongozi wa Klabu ya Singida Black Stars unapenda kuwajulisha wadau na mashabiki wetu kuwa tumeona taarifa zinazosambaa kuhusu maslahi ya mchezaji wetu Israel Patrick Mwenda tuliyemsajili msimu huu 2024/2025 kwa Ada ya TZS 200m. Makubaliano ya mkataba yaliweka kiasi cha pesa kinachotakiwa kulipwa kabla ya mchezaji kusaini ni TZS 140m ambacho klabu ilimlipa kama mkataba ulivyotaka, kiasi kingine kilichobaki TZS 60m kinatakiwa kulipwa muda wowote baada ya kukamilisha usajili. Huu ni utaratibu wetu kama Klabu na wapo wachezaji wengine waliopewa malipo ya utangulizi kabla ya kusaini na malipo mengine wanaendelea kupokea wakiwa wanaendelea na Ligi. Kuna wachezaji wamepokea malipo ya awali 20%, wengine 40% wengine 50%. Israel Mwenda amepokea 140m kama kiambatisho kinavyoonesha na anadai 60m. Yeye amechagua kusubiri mpaka alipwe kwanza ndio ajiunge na timu tofauti na wenzake ambao wanalipwa huku wakiwa kazini kama ilivyo kwenye vilabu vingi hapa nchini. Klabu itaendelea kufanyia kazi maslahi yake kwa mujibu wa makubaliano kwa kumalizia sehemu ya ada yake ya uhamisho iliyobaki ambayo inatakiwa kulipwa muda wowote baada ya kukamilisha usajili wake na mchezaji kujiunga rasmi na timu yetu. Uongozi wa klabu unamtaka mchezaji kuripoti kambini haraka kwa ajili ya maandalizi ya ligi inayoendelea kwa kuwa mahitaji yaliyobaki hayakuwa takwa la mkataba kuwa alipwe kwanza ndio aungane na timu kambini.

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par


Suivant