LIVE: MWEKEZAJI MZAWA ROUNDTABLE NDANI YA POWER BREAKFAST NA CLOUDS 360
Sekta ya uwekezaji Tanzania ni miongoni mwa Sekta zinazokua na kwa kipindi cha Mwaka uliopita wa Mwaka 2023 ukuaji wake umefikia asilimia 60, Kwa mujibu Kituo Cha uwekezaji nchini (TIC). Serikali imerahisisha uwekezaji Kwa wazawa Kwa kuweka Sheria inayorahisisha uwekezaji, ikiwamo kupunguza kiwango kwa Mwekezaji Mzawa kutoka Dola 100,000 (laki Moja) za Marekani za Awali hadi kufikia Dola 50,000 (elfu hamsini). Wakati ndoto ya Taifa ikiwa ni kumfanya Mwekezaji Mzawa kukua na kushindana Kimataifa, lakini bado hali hairidhishi, Nini kifanyike kutoka hapa na kusonga zaidi .. Kufanikisha ni kwenye collabo ya Power Breakfast na Clouds 360, Live kutokea Serena Hotel, Jijini Dar es salaam tukiwa na .... ⏭️ JOSEPH KUSAGA - Mkurugenzi Mtendaji Clouds Media Group. ⏭️ ROSTAM AZIZI - Mfanyabiashara. ⏭️ Balozi AMI MPUNGWE - Balozi. ⏭️ RAPHAEL MAGANGA - Afisa Mtendaju Mkuu TPSF.