Maafisa wa upelelezi wanachunguza mzozo wa umiliki wa ardhi
0
0
21/01/24
Watu watano wametiwa mbaroni kufuatia tuhuma za kughushi stakabadhi za kukodisha ardhi ya ekari 25 ya hospitali ya War Memorial iliyoko jijini Nakuru. Watano hao walitiwa mbaroni na maafisa wa jinai na kupelekwa katika ofisi za upelelezi wa jinai za eneo la bonde la ufa. haya yanajiri huku mvutano wa umiliki wa ardhi hiyo ukiendelea baina ya serikali ya kaunti ya Nakuru na usimamizi wa hospitali ya War Memorial.
Montre plus
0 commentaires
sort Trier par