Suivant

Magunia zaidi yenye mabaki ya miili yapatikana katika timbo ya Mukuru Kwa Njenga,

14/07/24
K24 TV
Dans Afrique / Kenya

Magunia mengine mitano iliyo na mabaki ya miili imepatikana katika timbo ya Mukuru Kwa Njenga, na kuongeza hofu kwamba uchunguzi unaweza kubaini miili mingine zaidi. hili likijiri baada ya ugunduzi wa karibu miili kumi hiyo jana. Makundi ya asasi za kiraia za kutetea haki za binadamu sasa yanataka uchunguzi wa haraka wa mauaji hayo. pia wanasisitiza usimamizi huru wa uchunguzi ili kuthibitisha sababu ya vifo katika kile kinachoshukiwa kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu. Pilka pilka za kuchukuliwa kwa magunia hayo na hii hapa taarifa yake.

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par


Suivant