Suivant

Maseneta wataka wabunge wakubali kupunguziwa mishahara

04/07/24
K24 TV
Dans Afrique / Kenya

Huku taifa likikumbwa na maandamano ya vijana ambayo kwa sasa yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 39, na kuacha mamia ya majeruhi na hasara ya mamilioni ya pesa , bunge la seneti leo limetoa mapendekezo yanayolenga kuishinikiza serikali kupanga mikakati itakayotuliza hali humu nchini. Maseneta wamepinga nyongeza ya mishahara na kutaka kuondolewa kwa taasisi kadhaa za serikali zikiwemo EACC, NCIC , ODPP na afisi za wake wa viongozi wakuu serikalini ili kupunguza mzigo wa mshahara.

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par


Suivant