Suivant

Mdhibiti wa bajeti adai turajie miujiza kuhusu malengo ya ushuru

17/05/24
K24 TV
Dans Afrique / Kenya

Mdhibiti wa bajeti Margret Nyakango ametofautiana na rais William Ruto hasa kuhusu makadirio ya kukusanya ushuru wa trilioni 2.9 katika mwaka ujao wa kifedha. Nyakango amesema KRA itaambulia patupu kwani lengo la kukusanya shilingi bilioni 700 zaidi ni la kutarajia miujiza, ikizingatiwa kile KRA itakusanya katika mwaka huu wa kifedha. vilevile nyakango amekashifu kiwango cha fedha ambazo zimetengezwa maendeleo ambacho ni bilioni 687 ikilinganishwa na matumizi ya kawaida ya shilingi bilioni 2.78 akionya kuwa uchumi hautaimarika kamwe.

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par


Suivant