Suivant

Mufti wa Tanzania: Zamani Mtoto Alikuwa Anaonywa na Jamii I Tunapokwenda ni Kuangamia kwa Taifa

05/07/24
CLOUDSMEDIA
Dans Afrique / Tanzanie

"Malezi ya zamani hayakuwa ya mtu mmoja yalikuwa ya mama, baba, kaka, dada, jamii, majirani, wazee wa mtaa mpaka shuleni lakini siku hizi hiyo hakuna. Mzee hawezi kukubali kupokelewa mzigo na mtoto anawaza utafika kweli huu? Mtoto alikuwa anaonywa na jamii nzima na watu wote na anaweza akapigwa akikosa adabu na mzee yoyote au kaka mkubwa yoyote na kwa sababu anajua ule ni utamaduni hasemi nyumbani maana anajua atapigwa zaidi. Kesho mtoto harudii. Na hata shule ilikuwa umefanya kosa au utundu mwalimu anakuadhibu na ukirudi husemi maana utapigwa tena na wazazi walikuwa wanawaamini waalimu na waalimu wanawaamini wazazi. Na wakatokea watoto wazuri, kizazi kilichokuwa bora chenye watoto wanaojitambua wanatakiwa wafanye nini." - Sheikh Abubakar Zubeir - Mufti wa Tanzania akizungumzia Kitabu chake cha 'Mmomonyoko wa Maadili Nani Alaumiwe?' #LiveOnClouds360 #CloudsTvNiMkataba

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par


Suivant