Muungano wa wauguzi na wakunga (KNUN) watoa ilani ya mgomo ifikapo januari 13
0
0
24/12/24
Muungano wa wauguzi na wakunga humu nchini (KNUN) umetoa ilani ya mgomo ifikapo januari 13 ikiwa serikali itashindwa kushughulikia matakwa yao. muungano huo umelalamika kuhusu uhaba wa wauguzi, kutotekelezwa kwa mkataba wa makubaliano ya pamoja wa mwaka wa 2017, kutopandishwa kwa vyeo pamoja na masuala mengine. wakati huo huo, muungano wa wataalamu wa afya ya mazingira na maafisa wa afya ya umma humu nchini wameonya wananchi kuwa huenda wanakula chakula kilicho na kinyesi na hata madini ya zebaki yaani mercury. Wataalamu hao pia wametishia kugoma mwezi januari ikiwa serikali haitawapa kipaumbele katika mgao wa fedha, uajiri wa maafisa wa afya wa umma pamoja na masuala mengine.
Montre plus
0 commentaires
sort Trier par