Mwabukusi: Elimu ya Sheria Lazima Iboreshwe I TLS Haitumiki & Wapinzani, Sina Mpango wa Kugombea
"Kulikuwa na changamoto na ushindani mkubwa wakati wa uchaguzi na hii ni kwa sababu ya imani kubwa watu waliyonayo katika chama na changamoto ilichochewa na mfululizo wa mapingamizi niliyokuwa nikiyapata kwa sababu nilianza kupata mapingamizi toka ndani ya chama kuwa nisigombee, sina sifa, nikashinda pingamizi la kwanza muhusika akakata rufaa nikashindwa kwenye mazingira ya ajabu kidogo. Kwanza ile kamati ya Rufaa ilijigeuza na kuwa kama Mahakama wakajipa mamlaka ambayo haina na wakaniondoa bila kunisikiliza yaani waliibua jambo, wakalijadili na kuliamua hata kupinga ilikuwa ngumu na wakaniondoa kuwa sina sifa jambo ambalo likanilazimu kwenda mahakamani. Tunapambana mahakama kuu nashukuru Mahakama ikasema nina haki ya kugombea na kamati ya Rufaa ilikosea ikanirejesha. Ulikuwa uchaguzi wenye ushindani." - Boniface Mwabukusi - Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika #LiveOnClouds360 #AsantekwaTafuu