Suivant

Onyo la KUPPET kuhusu muhula wa tatu

20/07/24
K24 TV
Dans Afrique / Kenya

Chama cha walimu wa shule za upili , KUPPET, kimeapa kuwa shule hazitafunguliwa kwa muhula wa tatu hapo Septemba, endapo ndani ya siku 7, serikali haitakuwa imetekeleza matakwa yao. Baadhi yazo ni kuajiriwa na kulipwa kwa walimu wa JSS elfu 46 na wengine watarajali elfu 20 mwezi huu, utekelezaji wa mkataba wa makubaliano ya pamoja wa 2021/25, pamoja na kuwepo kwa bima ya afya kwa walimu. Hayo yakijiri, katibu wa wizara ya elimu belio kipsang amelalamikia kiwango kidogo cha ufadhili wa serikali, kuondolewa kwa bajeti ya ujenzi wa madarasa na kuondolewa kwa bajeti ya lishe bora. hatari iliyoko endapo bajeti ya ziada iliyo na upungufu wa ufadhili itapitishwa ilivyo.

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par


Suivant