Suivant

Prof Janabi Azindua Mashine Mpya Ya Saratani

18/04/24
CLOUDSMEDIA
Dans Afrique / Tanzanie

Hospitali ya Taifa Muhimbili leo imezindua mashine mpya ya kisasa (Senographe Pristine 3d Mammography suite) yenye thamani ya TZS. 800 MIL yenye uwezo mkubwa wa kufanya uchunguzi wa saratani ya matiti kwa njia ya kisasa zaidi. Akizindua mashine hiyo kwa niaba ya Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Tiba Wizara ya Afya Dkt. Hamad Nyembea amesema mashine hiyo ni ya kwanza kufungwa hapa nchini na inauwezo wa kufanya uchunguzi kwa njia ya kisasa zaidi tofauti na mashine zilizokuwa zinatumika awali. Ameongeza kuwa mashine hiyo inauwezo wa kufanya uchunguzi wa Saratani ya Matiti zinazotoa picha za kawaida (2D Mammography) pamoja na huduma za kiuchunguzi za saratani ya matiti zinazotoa picha nyingi zaidi kwa kipimo kimoja (3D Mammography) ambazo humrahisishia kwa haraka mtaalam kusoma na kufanya maamuzi ya kimatibabu. “Mashine hii pia inauwezo wa kufanya uchunguzi wa kibobezi (Specialized images) ambapo mgonjwa huchomwa sindano ya dawa ambayo wakati wa kupiga picha dawa hiyo hujikusanya kwenye maeneo yanayohisiwa kuwa na shida pamoja na kuwaongoza wataalam katika kutoa kinyama kwenye matiti kwa ajili ya uchunguzi zaidi” amesema Dkt. Nyambea Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema saratani ya matiti ni tatizo kubwa nchini Tanzania ambapo takwimu zinaonesha kuwa hii ni saratani ya pili kwa wanawake katika nchi yetu na inaendelea kuongezeka. Pamoja na hayo ameishukuru Serikali ya Marekani kupitia Jumuiya ya Radiolojia ya Amerika ya Kaskazini na GE Healthcare kwa kuwezesha upatikanaji wa mashine hiyo ambayo itaenda kuleta mapinduzi katika sekta ya afya nchini. #CloudsDigitalUpdates

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par


Suivant