Rais Ruto aendelea kutetea mpango wa serikali wa kutoa chanjo kwa mifugo
0
0
11/12/24
Rais William Ruto ameendelea kutetea mpango wa serikali wa kutoa chanjo kwa mifugo ambao umeendelea kupata pingamizi kutoka wadau. Rais amewataja wanaopinga mpango huo kama watu wasio na akili timamu. akizungumza katika kongamano la uongozi wa jamii za wafugaji katika kaunti ya Wajir, Rais amesema mpango huo ni muhimu katika kudhibiti kuenea kwa magonjwa na kufungua soko la kimataifa la bidhaa za mifugo nchini Kenya.
Montre plus
0 commentaires
sort Trier par