Suivant

Rais Ruto atetea hatua ya Kenya kuingia mkataba na kampuni ya Adani

03/10/24
K24 TV
Dans Afrique / Kenya

Rais William Ruto ,ametetea hatua ya kenya kuingia mkataba na kampuni ya Adani ili kupewa usimamizi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa jomo kenyatta, akisema hilo litainua hadhi ya uwanja huo kote duniani. Rais amezungumzia swala hilo kwa mara ya kwanza hii leo katika maonyesho ya kitalii ya bustani ya Uhuru, akisisitiza uamuzi huo utapiga jeki kenya kama kitovu cha utalii, kwa mujibu wa rais, ukarabati wa jkia utafanya uwanja huo uwe na uwezo wa kupokea wasafiri milioni tano kila mwaka ifikiapo mwaka 2027.

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par


Suivant