Serikali ya Ruto katika mwaka wake wa kwanza wa kifedha ilitaka kutumia shilingi bilioni thelathini
Imebainika sasa kuwa serikali ya rais William Ruto katika mwaka wake wa kwanza wa kifedha ilitaka kutumia shilingi bilioni thelathini ambazo hazikuwa kwenye bajeti katika kile kinachosemekana kuwa ni fedha za dharura. Hata hivyo mdhibiti wa bajeti margaret nyakang'o alikataa kuidhinisha kiasi hicho cha pesa kutokana na ukosefu wa sababu muafaka lakini aliidhinisha shilingi bilioni 19. kinachobua masuali ni uwezekano wa kutumika vibaya kwa kifungu cha katiba cha mia mbili ishirini na tatu kwa mfano serikali kutaka bilioni moja kupanga sherehe ya madaraka iliyofanyika Bungoma licha ya kuwa sherehe hizo hufanyika kila mwaka na zinapaswa kujumuishwa katika bajeti. Sasa anatueleza kuwa kamati ya fedha bungeni inapania kuziba mianya ya utumizi mbaya wa kifungu hicho kinachoruhusu fedha kutumika kwanza kabla ya bunge kuidhinisha.