Serikali za kaunti bado zinapuuza taratibu zilizowekwa kisheria
0
0
31/07/24
Mdhibiti wa bajeti Margaret Nyakang’o amebaini kwamba serikali za kaunti bado zinapuuza taratibu zilizowekwa kisheria na mapendekezo ya afisi na hivyo kuepuka uwajibikaji. Nyakang’o aliyehudhiuria warsha ya maseneta wenyeviti wa kamati mbalimbali katika bunge la seneti pia amependekeza kuongezwa kwa bajeti ya afisi yake ili itekeleze kikamilifu wajibu wa kulinda matumizi ya pesa za umma. Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi amefungua rasmi warsha hiyo ya siku tatu.
Montre plus
0 commentaires
sort Trier par