Suivant

TANZIA: DIDA Shaibu wa Wasafi FM Afariki Dunia!

04/10/24
CLOUDSMEDIA
Dans Afrique / Tanzanie

Kwa masikitiko makubwa tumezipokea taarifa za kifo cha Khadija Shaibu maarufu kama Dida aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha @WasafiFM Kipindi cha Mashamsham. Taarifa za awali zinaeleza mauti yamemfika Dida usiku huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alikuwa amelazwa na kupatiwa matibabu. Tasnia ya Habari itamkumbuka Dida kwa umahiri wake katika uongozaji wa vipindi vya Radio akisimama kama kioo kwa Wanawake wengi hapa nchini, tunatambua na kuthamini mchango wake mkubwa katika tasnia hii. Kama CLOUDS tunatanguliza salamu za pole kwa Wasafi Media kwa kuondokewa na Mtangazaji huyu mahiri, Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote. Dua na sala zetu ziko pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu. ???????? Innalilahi wa inna ilaihi rajiun. •

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par