ULEGA AKAGUA MIRADI UJENZI WA BARABARA DAR
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega leo amefanya ziara ya ukaguzi ujenzi unaendelea wa barabara na miundombinu wa mradi wa mwendokasi (BRT 3) jijini Dar es salaam. Ziara ambayo ilianzia makao makuu ya TANRAODS, posta ya zamani mtaa wa Azikiwe hadi Nyerere road Gongo la mboto. Mhe. waziri Ulega amefurahishwa na kuwapongeza wasimamizi wanaofanya kazi ya kuwa simamia wakandarasi wanaofanya kazi katika eneo la barabara ya Nyerere. Waziri anukuriwa akisema “wakandarasi wamekwenda sawa na matakwa ya mkataba wetu”. Pia Mheshimiwa waziri ametoa maelekezo ya barabara yote ya Nyerere iwekwe taa haraka zoezi liende sambamba na ujenzi wa barabara yenyewe. Pia Mheshimiwa Waziri atoa neno juu ya changamoto ya foleni inayoendelea jijini Dar es salaam kwa wasimamizi waweze kutatua changamoto hiyo kwa kuwezesha kuruhusu maeneo ambayo ujenzi wake umekamilika waruhusu watu waanze kupita hili kupunguza tatizo la foleni. Mwisho Mheshimiwa Waziri amewapongeza Watanzania na wanadar es salaam kwa uvumilivu wao katika kipindi hiki cha ujenzi wa miundombinu hiyo maana kazi inayofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ni kazi njema yenye nia ya kutaka kuondosha kabisa changamoto ya foleni jijini Dar es salaam.