Waathiriwa waibuka na kudai mshukiwa wa mauji ya Starlet Wahu, aliwai wadhulumu akitaka kuwaua
0
0
06/01/24
Maafisa wa polisi wanachunguza kubaini iwapo mshukiwa aliyehusika mauaji ya Starlet Wahu Mwangi alikuwa muuaji wa kulipwa au ni gaidi. Lakini mshukiwa huyo john matara anadai Starlet amekuwa rafikiye wa kike kwa kipindi cha miaka miwili. Polisi wana kibarua kubaini iwapo mshukiwa anasema ukweli ama alimlenga msichana huyo kwa lengo la kumuathiri. Aidha msichana mwenyewe amezikwa leo huko Kamulu, wengi wakibaki na maswali chungu nzima. Aidha polisi wamearifu K24 kunaye msichana mwengine ambaye amefika kituoni Industrial Area kuripoti kuhusu tukio lingine sawa na hili linalohusu mshukiwa John Matara.
Montre plus
0 commentaires
sort Trier par