Suivant

WANA CCM TUSISALITIANE | KWENYE UCHAGUZI WA SASA HAKUNA RUSHWA

16/07/24
CLOUDSMEDIA
Dans Afrique / Tanzanie

Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa na Mkurugenzi wa Taasisi za Furaha, Furaha Dominic amesema kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika October mwaka huu CCM imejipanga kuhakikisha haipotezi nafasi hata moja. Furaha amesisitiza kuwa CCM itapeleka wagombea wanaokubalika huku akiwaomba wanachama kuungana ‘tutawapima viongozi kwa utendaji kazi wao na kukubalika kwao ndani ya jamii niwaase wana CCM wenzangu pale anapochaguliwa mtu anayekubalika tusisalitiane tuungane kukitetea chama’. Kada huyo wa CCM ametoa mtizamo wake kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa akiwa Jijini Dar es asalaam aliposhiriki kampeni ya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura katika tawi la CCM Komba lililopo katika Jimbo la Kawe.

Montre plus

 0 commentaires sort   Trier par


Suivant